M Mafole Baraka
EN SW
Log in Changia
Jinsi ya kupata namba ya Marekani kwa ajili ya kuverify platform ambazo hazifanyi kazi Tanzania.

Jinsi ya kupata namba ya Marekani kwa ajili ya kuverify platform ambazo hazifanyi kazi Tanzania.

August 15, 2026 · 3 min read

Marekani ni moja ya nchi yenye advantage kubwa linapokuja kwenye michongo ya mtandaoni.Platforms nyingi za kufanya kazi mtandaoni huwa zina feature za ziada kwa wakazi wa Marekani na nyingine huenda mbali kwa kuwalipa wakazi wa marekani pekee.

Platform kama Tiktok huwa inawalipa creators wa Marekani kulingana na idadi ya views wanaopata wakazi wa Marekani na pia huwa wana features za ziada kama Tiktok shop kwa wakazi wa Marekani.

Mbali na akaunti za mitandao ya kijamii, Platforms za kufanyia kazi mtandaoni hususani kazi za kutrain AI models huwa hazikubali no za Tanzania wakati wa utoaji wa OTP hali inayopelekea vijana wengi kukosa fursa ya kufanya kazi na platforms hizo.

Kwenye makala hii nitakuelezea kwa undani namna rahisi na ya bei nafuu ya kupata namba ya Marekani kwa ajili ya kuverify OTP kwenye platforms ambazo hazifanyi kazi bongo.

Kabla hatujaenda moja kwa moja kwenye platforms za kupata no ya US ya kuverify akaunti mbalimbali haya ni mambo ya muhimu ambayo ningependa ufahamu kwanza.

Jinsi ya kupata no ya kuverify platforms mbalimbali za US

kuna Platfroms nyingi ambazo zinatoa no za marekani kwa ajili ya kuverify OTP kwenye platforms mbalimbali, baadhi ya platform hizo ni pamoja na quo, Tello na VOIP.

Hizo nimetaja hapo juu ni baadhi ya platform za kupata no za US na binafsi nisingependa kuzungumzia platforms ambazo sijawahi jaribu. Kwenye article hii nitazungumzia platform inayoitwa text verify, platform ambayo nimewahi kutumia kuverify akaunti kwenye platforms mbalimbali.

Text verify inafanyaje kazi?

Moja ya changamoto kubwa unayoweza kukumbana nayo baada ya kununua no ya marekani ni pale utakaponunua no ya marekani kisha uombe OTP na ushindwe kuiona kwenye inbox ya namba ambayo umenunua.

Kwa Text verify jambo hilo sahau kukumbana nalo kwani kabla hujaomba no ya kupokelea OTP wao wanakuuliza kabisa ni platform gani unayotaka kupokelea OTP so incase hutoniona hiyo platform maana yake hiyo platform huwezi kuitumia text verify kuombea OTP.

So kwa maelezo mafupi, Text verify inakusaidia kupata OTP kwenye platform baadhi na kwenye kila platform unayoombea OTP lazima ulipie kiasi kidogo ambacho huwa hakifiki hata tsh 500.

Jinsi ya kufungua akaunti ya text verify