Nimeanza kuingiza hela mtandaoni kwa kupitia kazi za translation mwaka mmoja tu baada ya kumaliza kidato cha sita.Hadi leo naikumbuka hiyo kazi na uzuri kwenye kupekua pekua nimeikuta kwenye emails zangu.
Andiko hili nitashare hadithi yangu, kwa upande wa kazi za translation pekee.Hakikisha unasoma kila neno, kila nukta, ahdi mwisho.Kuna mengi sana utajifunza.

Kazi yangu kubwa hapo ilikuwa ni kusikiliza audio ya sekunde kadhaa ya kiingereza kisha nitafsiri kwenda kiswahili then nirekodi audio ya yale matamshi kwa kiswahili.
Kitu sikuwa najua ni kwamba huu ulikuwa mwanzo wangu wa kuingiza $ 10k+ kwa kutafsiri kutoka kiingereza kuja kiswahili.

Siku chache zilizofuata nikapata mteja mwingine, na huyu alikuwa na budget ya $300 kwa kazi ya kutafsiri makala mbalimbali kutoka kiswahili kuja kiingereza. Bahati mbaya mteja huyu aliishia kunilipa $5 pekee kwani kuna moja ya kosa kubwa sana nilifanya.

mteja alikuwa analipa kwa kila Milestone( Milestone ni unalipwa hatua kwa hatua), na step ya kwanza kabisa ya malipo yake ilikuwa ni analipa $5 kwa kila article utatafsiri.Time hiyo nilikuwa busy field, so nikatafuta mtu anifanyie na uzuri alinifanyia kazi ila bahati mbaya sikuikagua kabla sijamtumia client.
Client hakuapprove ile kazi na hapo ndipo nilipishana na $300 yangu ya kwanza ya online.Mwili wangu ulitetemeka sana nikidhani dunia ndio inaisha hapo. Hela nilikuwa nishaipigia mahesabu maskini ya mungu.

Client huyo aliniandikia review mbaya sana, review ambayo hakuna client ambaye angefuata angetaka kufanya kazi na mimi.Mind you, hapo nilikuwa na miezi michache tangu nimalize kidato cha sita hata mambo ya kuandika emails na vitu vingine siwezi.
Incase unadhani pilika pilika zangu mtandaoni ziliishia hapo basi unajidanganya kwani sikukoma kutafuta fursa za kazi za utafsiri mtandaoni.
Safari hii nikasema nazifuata kazi zinapotokea na huko huko wakiamka wataamka na emails zangu.Na moja ya kitu nilifanya ni kuanza kutuma emails kwa agaency mbalimbali, nilituma kwa agency zaidi ya 100 ila hapa nistashare chache tu.
Email yangu ya kwanza kabisa nilituma kwenye agency ya UK na haya ndo majibu walinipa.

Hapo sikuwa na experience hata jibu nililompa hakulikubali so ndio nilipishana na huyu client, natamani sana kipindi hiki ningekuwa na mtu wa kunishika mkono.
Then nikapata client mwingine, ila huyu alikuwa wa Canada, na akanighost.Imagine experience yako ya kwanza ya kuwa Ghosted ni ya client na sio ya mpenzi wako.

Nikatuma kwa client mwingine wa India ila hapa sadly project ilikuwa imeisha so ni kama nilikuwa nimechelewa kumtumia email.

Client wengine wakaniletea story za kunifanyia assesment kwanza na nikiwa mkweli, kwa kipindi kile ni ngumu sana kwangu kufanya assesment kwa ni hata lugha ya mkoloni kwangu ilikuwa ngumu sana kuiongea.

But kama maandiko ya dini yanavyosema, wakati wangu wa kubarikiwa ukafika sasa na wateja wakaanza kumiminika upande wangu.
Client wa kwanza akakubali kunilipa ila pumbavu mimi niliweka nilipwe kidogo kwa neno $0.04 kwa neno.

Safari ikaenda hadi nikapata wateja wa kunilipa $800+ kwa project (Inshort niko na screenshot nyingi sana ila najua hamtoziangalia so hizo ni sample tu).

Ukisoma kwa makini andiko hili utagundua
Kazi za translations ziko nyingi sana changamoto ni sehemu za kuzipata.
Kama hujui namna bora ya kuandika proposal ni ngumu sana kupata hizi kazi.
Kwa kuligundua hilo nimendaa document (database) ambayo ina
Agency 100 zinazotoa kazi za translations kwa freelancers ( Jina la agency na link ya websites zao zipo)
Tools zinazotumika kufanya translation.
Sample email ya kuwatumia watoa kazi za translation
List ya vendor managers wa linkedin na link za profile zao za linkedin
Sample proposal za Upwork kwa kazi za translation
Jinsi ya kuipata hiyo document
Kama uko Tanzania unaweza ipata kupitia link hii: https://flutterwave.com/pay/kazizatranslation
Kama uko nje ya Tanzania unaweza ipata kupitia link hii: https://barakamagic.gumroad.com/l/Translationagencies
Hii ni part 1 tu, part ya pili nitawaeleza vingi zaidi.Huwa ninasoma comment pia, mnaweza niandikia chochote nami nitawajibu.
Usiache kutembelea link hii: https://liinks.co/mafolebarakatz