Billboard ni moja ya chati kubwa ya muziki duniani na karibu kila msanii ulimwenguni huwa anatamani siku moja awe kwenye chati za Billboard.Kundi kubwa la wasanii ambao nyimbo zao zinapata nafasi kwenye chati za Billboard ni wale ambao aidha wako chini ya lebo kubwa ama wana kiasi kikubwa cha fedha wamewekeza kwenye kutangaza kazi zao na hata kwenye production.

Dunia zimebadilika sana hususani kutokana na teknolojia, Huenda utamaduni wa kutumia bajeti kubwa kwenye kutengeneza muziki mzuri ama kutumia bajeti kubwa kutengezeza video za muziki huenda umepitwa na wakati ama unaelekea kupitwa na wakati.

Miezi michache iliyopita msanii wa AI, Xania Monet aliingiza nyimbo zake kwenye chati ya Billboard na kusaini deal la dola za kimarekani milioni 3. Wiki hii pia, mtengeneza maudhui maarufu wa Tanzania Temidayo alitangaza EP ya pili ya msanii wake wa AI aitwaye Taliyah. Mifano iko mingi sana kuhusu wasanii wa AI kwani hata Nigeria msanii Fave baada ya kuachia nyimbo yake ya intentions, mtaalamu wa AI akatengeneza AI version ya wimbo huo ambao ulipata engagement kubwa kuliko nyimbo original hali iliyopelekea Fave kuamua kufanya remix na msanii huyo wa AI.

Mbali na story hizo ambazo kwa namna moja ama nyingine ni nzuri sana kuisoma ama kusikia kupitia vyombo vya habari, lakini ushawahi jiuliza huwa wanatumia nini kutengeneza wasanii wa AI na kuupload nyimbo za wasanii hao kwenye majukwaa ya kidijitali na kujiingizia kipato?

Soma makala hii kufahamu namna ambavyo wasanii wa AI huwa wanatengenezwa na namna ambavyo wasanii wanaingiza kipato kwa kutumia wasanii wa AI

Angalizo: Baadhi ya link kwenye makala hizi ni affiliate na nitalipwa commision kidogo utakapojisajili na huduma hizo kwa kupitia link nimeziweka hapo.

man in black t-shirt playing guitar

Kabla hatujaenda moja kwa moja kwenye namna gani unaweza kutengeneza msanii wako wa AI na kuanza kumtumia kupata hela, zifuatazo ni dondoo chache ambazo ningependa ufahamu

  • Anzia youtube: Unapokuwa umemtengeneza msanii wako wa AI moja ya sehemu nzuri ya kuanzia ni Youtube, zifuatazo ni sababu za kwanini nafikiria youtube ni sehemu sahihi ya kuanzia

-Youtube inakupa nafasi ya kumjaribu msanii wako kwenye staili tofauti tofauti za muziki. Platform za kusambaza muziki kama distorkid na Tunecore haziko flexible especially kama ndio unajitafuta na hujaamua msanii wako kama aimbe gospel, Mchiriku ama Rnb.

-Youtube kutumia na kuupload kazi zako za muziki ni bure kabisa hivyo hutolazimika kuingia gharama kubwa wakati unamtaarisha msanii wako kuingia sokoni na wakati mwingine msanii wako akiingia mjini vizuri unaweza kuingiza hela mapema kabisa.

- Kupata mashabiki Youtube ni rahisi sana kuliko kupata mashabiki kwenye platforms zingine so ni muhimu sana uanzie kutengeneza audience huko halafu majukwaa mengine yafuate.

  • Tengeneza biography ya msanii wako: Kibongo bongo tunaweza kusema mbrand msanii wako ama mtengenezee kiki. Unaweza kufanya hivyo kwa kuwaomba watu maarufu ambao una ukaribu nao wakusaidie kumposti msanii huyo kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii ama bloggers wamzungumzie. Kwa sasa una advantage kwani ni watanzania wachache sana wana msanii wa AI so kupata shavu ya msanii wako kuzungumziwa hususani kama ana ngoma kali ni rahisi sana.

  • Tengeneza nyimbo zako original: Changamoto ya watu wengi wenye wasanii wa AI huwa wanawatumia kutengeneza cover na remix za wasanii wengine ambao tayari wana soko kwenye kiwanda cha muziki. Wasanii wengi huwa wamewekea hakimiliki nyimbo zako hivyo kutengeneza remix ama cover za nyimbo za wasanii wengine inaweza kupelekea akaunti yako kufungiwa ama kutooneshwa kwa watazamaji na wasikilizaji wako

Nawezaje kutengeneza msanii wangu wa AI?

fuata hatua zifuatazo kutengeneza msanii wako wa AI

  • Mtafutie jina msanii wako: Hiki ni kitu cha kwanza kabisa ambacho unatakiwa ufanye, mpe jina la kisanii msanii wako kulingana na mziki unaotaka aufanye. Nitashangaa sana msanii wako umuite “Mafole” halafu awe anaimba RnB, but sitoshangaa ikiwa huyo msanii ukamuita “Mafole” halafu akawa anaimba nyimbo za kiasili.

  • Mpeleke studio msanii wako: Kibongo bongo ningekwambia mpeleke msanii wako wa S2KIZZY ama kwa T Touch au kwa Dj Mushizo, lakini kwa ai studio yako ni moja tu inaitwa Suno AI. Kupitia suno AI unaweza kumtengenezea msanii wako aina yoyote ya nyimbo unayotaka atengeneze.

  • Mtengenezee photoshoot msanii wako: Wasanii wengi ulimwenguni kitu cha kwanza ambacho huwa wanasifiwa nacho ni namna mionekano yao inavyokuwa hivyo ni muhimu sana msanii wako wa AI awe na muonekano mkali unaweza kutumia Google Gemini, Google nano banana ama Chat Gpt kutengeneza munekano wa msanii wako.

  • Mfungulie akaunti ya mitandao ya kijamii: Hakikisha msanii wako anawadatisha watu mtandaoni kwa kuhakikisha unamtengenezea akaunti kwenye kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii kama vile Instagram na Tiktok na hakikisha video na picha anadondosha huko zinadatisha watu.

  • Mtengenezee kichupa kikali: Kwenye dunia ya sasa video kali ndio kila kitu, kibongo bongo mtu kama Director Kenny ama Majag ningesema wahusike kwa wapopo kule ningesema labda Director Pink ama Meji Alabi ndio wahusike ila huku kwenye AI wewe mwenye msanii ndio director na tool kama Sora AI na Google Veo 3 ndio utatumia kumtengenezea video kali msanii wako.

  • Piga PR na marketing kali: Inshort mtafutie kiki msanii wako wa AI, mtafutie mchumba, muimbishe nyimbo trending za wakati huo, fanya kila unachoweza watu wamjue.

  • Sambaza nyimbo za mssanii wako kwenye majukwaa ya muziki kama Spotify na Apple Music: Moja ya kitu utakuwa shocked ni namna gani ni rahisi kusambaza nyimbo kwenye majukwaa ya muziki kama vile Spotify, Audiomack na Apple Music. Tumia tool kama vile Distrokid na Tunecore kusambaza nyimbo za msanii wako kwenye majukwaa ya muziki.

Suno AI ni nini na inafanyaje kazi?

Suno AI ni tool ya AI inayotumika kutengeneza nyimbo mbalimbali za AI.Almost 80% ya nyimbo za AI zinazopatikana mtandaoni kwa sasa zimetengenezwa kwa kutumia Suno AI.

Msanii wako wa AI unaweza mtengenezea style yeyote ya nyimbo unayojiskia wewe na kwa kutumia lugha yeyote ambayo wewe unajiskia. Unaweza mtengenezea lyric msanii wako kisha ukamwambia aimbe, unaweza muacha ajitengenezee lyrics yeye mwenyewe aimbe na unaweza mchagulia style ya kuimba ama umuache ajichagulie yeye mwenyewe.

Fuata hatua hizi kutengeneza akaunti ya SUNO AI

  • Fungua akaunti akaunti ya Suno AI, Suno wana app playstore na App store.

  • Utaona sehemu imeandikwa Create, hapo unaweza tengeneza nyimbo zako za majaribio.

Mwisho, Tools nyingi nimezitaja hapa itakubidi ulipie kiasi kidogo ndio uweze kuzitumia, kama uko serious na msanii wako tenga bajeti kidogo kufurahia muziki wake. Ikiwa umependa andiko hili kuna huduma mbalimbali ambazo huwa natoa unaweza kuzitazama kwenye link hii https://liinks.co/mafolebarakatz