Moja ya changamoto kubwa tunayopitia watu tunaoanza kujitafuta kwa kufanya kazi mtandaoni ni namna gani tunaweza kupokea malipo mtandaoni. Kwa miaka mingi njia kubwa na maarufu za kupokea malipo kama vile Stripe na Paypal hazifanyi kazi Tanzania na hata nyingi zinazofanya kazi kama Payoneer zina makato makubwa.
Kwa sasa hali ni tofauti kidogo, ingawa changamoto za makato na rates kuwa ndogo bado zipo kwa freelancers wengi lakini kidogo tuna njia nyingi za kupokea malipo pale ambapo utapata mteja wa kufanya naye ambaye hayupo Tanzania.
Platform kama vile Grey, Wise na Raenest wamerahisisha namna freelancer waliopo Tanzania wanaweza kupokea malipo yao hususani kutoka kwa wateja ambao wanatokea mabara mengine kama vile Ulaya na Amerika.
Angalizo: Baadhi ya link kwenye makala hizi ni affiliate na nitalipwa commision kidogo utakapojisajili na huduma hizo kwa kupitia link nimeziweka hapo.
Kwanini uwe na akaunti za benki za Marekani, Uingereza na Ulaya?
Majukwaa mengi ya kufanya kazi mtandaoni yametengenezwa hususani kwa watumiaji ambao wanapatikana nchi za ulaya na Amerika, hivyo mengi njia pekee wanayotumia kufanya malipo ni moja kwa moja kwenda kwenye akaunti za benki za nchi husika na sio kuja moja kwa moja kwenye benki zetu za nyumbani kama vile CRDB na Selcom.
Kwa majukwaa ya kufanya kazi mtandaoni ambayo yanaruhusu kutuma fedha online moja kwa moja kuja Tanzania kwa njia ya wire yana makato makubwa ya kuanzia $30 - $50 kwa kila muamala utakaoufanya hivyo kufanya njia ya kutuma fedha moja kwa moja kuja kwenye akaunti za benki za nyumbani kuwa sio bora.
Vitu gani natakiwa kuwa navyo kabla sijafungua akaunti ya benki ya Marekani, Uingereza na Ulaya?
Platform nyingi zinazotoa akaunti za benki za Marekani, Uingereza na Ulaya huwa zinahitaji uwe na kitu kimoja ama viwili kati ya vifuatavyo
Kitambulisho cha kupiga kura
Kitambulisho cha uraia mf NIDA
Leseni ya udereva
Bank statement
Risiti ya malipo ya bili
Vitu vya muhimu vya kufahamu linapokuja suala la kufungua akaunti za benki za marekani, Uingereza na Ulaya
Kwa sasa Platform ya Wise haitoi akaunti za benki ya US kwa watanzania.
Akaunti za benki za US huwa zinatofautiana kuna ambazo zinaruhusu kupokea hela kwa ACH na kuna ambazo zinapokea kwa Wire pekee, Zinazopokea kwa ACH huwa zina makato nafuu na malipo yake huwa ya haraka zaidi so please hakikisha unakuwa nayo ya aina hii.
System za usalama za platform nyingi za kupokea malipo huwa sensitive na mara nyingi huwa wanauliza chanzo cha hela so kama hela yako ina makando makando kuna possibility kubwa ya hela yako kurudishwa.
Usimlipe mtu hela akutengenezee akaunti ya benki ya Marekani, Uingereza na Ulaya, jikaze tengeneza mwenyewe ni kitu ambacho unaweza kufanya ndani ya dakika tano.
Kuna tofauti gani kati ya akaunti ya benki ya Marekani na akaunti ya benki ya USD inayotolewa na benki za Tanzania?
Hiki ni moja ya kitu ambacho kinawachanganya watu wengi sana, wengi wetu huwa hatuwezi kutofautisha kati ya akaunti za benki za US za USD na akaunti za benki za USD zinazotolewa na benki za hapa nyumbani.
Akaunti za benki za USD za US ni zile akaunti za benki ambazo huwa zinatolewa na taaasisi za fedha ambazo zina makazi makuu ya US hivyo zinakupa address za huko kabisa huku akaunti za benki za USD zinazotolewa na mashirika ya fedha ya nyumbani ni akaunti ambazo zinakusaidia kuhifdhi na kutumia fedha ambazo ziko kwenye sarafu ya USD lakini address na vitu vingine vyako vinabakia kuwa Local.
Ukiwa na akaunti ya benki ya US inakurahisishia kupokea malipo kwa wateja wa Marekani kwani inakuwa kama vile wanamtumia fedha mtu ambaye wanakaa naye mji mwingine.
Soma pia: Jinsi ya kupata namba ya Marekani kwa ajili ya kuverify platform ambazo hazifanyi kazi Tanzania.
Nawezaje kutengeneza akaunti ya benki ya Marekani, Uingereza na Ulaya nikiwa Tanzania?
Kwenye sehemu hii nitatumia Grey(Tumia referall code ya “Y27DRO” unapofungua akaunti) kama program ya mfano ya kufungulia akaunti ya benki ya Marekani, Uingereza na ulaya.
Namna ya kufungua akaunti ya benki ya US, Ulaya na Uingereza kwa kutumia Grey
Sajili akaunti yako ya benki ya Grey: Tembelea tovuti ya Grey ama pakua App yako kupitia Playstore ama Appstore ila lazima uwe na email na namba ya simu ndio uweze kufungua akaunti.
Thibitisha utambulisho wako: Grey watakuuliza documents chache kama vile Kitambulisho cha serikali kama vile passport na NIDA, Utambulisho wa makazi yako mfano statement yako ya benki ama malipo yako ya bili.
Selfie: Kupitia program iliyopo kwenye App utatakiwa upige selfie yako moja ili wahakikishe kama details ambazo umewapa zinaendana na namna sura yako inaendana.
Omba akaunti za USD, EUR na GBP. Ukishathibitisha utambulisho wako hatua inayofuata ni kuomba akaunti ya benki unayoihitaji, unaweza kufanya hivyo kwa kuingia sehemu imeandikwa “accounts” kisha “Request a bank account” hakikisha unarequest akaunti ya benki ya kila sarafu ambayo ulikuwa unataka.
Mwisho, Mara nyingi inachukua hadi masaa 24 kupata akaunti yako ya benki. Unaweza kujifunza vitu mbalimbali kutoka kwangu kupitia link hii https://liinks.co/mafolebarakatz