African healthcare professionals using digital health technology in a clinical setting

Ukiwa healthcare professional, kuna vitu ambavyo tayari unavijua vizuri.

Unajua kuongea na patients.

Unajua medical terminology.

Unajua kufanya assessment, documentation, patient education au kufanya kazi ndani ya healthcare team.

Lakini kuna swali jingine ambalo healthcare professionals wanahitaji kuanza kujiuliza:

Je, nina digital skills zinazohitajika kwenye healthcare ya sasa?

Kwa sababu healthcare inabadilika.

Si kwamba technology inakuja kuchukua nafasi ya healthcare professionals. Badala yake, technology inabadilisha namna healthcare inavyotolewa, kusimamiwa, kurekodiwa na kuwasilishwa kwa patients.

WHO’s Global Strategy on Digital Health imeongezwa hadi 2027, ikisisitiza matumizi ya digital technologies katika kuimarisha health systems na kuboresha health outcomes.

Hii ina maana kwamba digital health siyo tena topic ya watu wa IT pekee.

Ni sehemu inayogusa pia healthcare professionals.

Digital health ni nini?

Digital health ni matumizi ya digital technologies kusaidia kuboresha afya na healthcare.

Inaweza kuhusisha vitu kama:

  • Electronic health records

  • Telehealth na telemedicine

  • Digital health applications

  • Health information systems

  • Remote patient monitoring

  • Digital patient education

  • Healthcare data systems

  • Artificial intelligence katika healthcare

Lakini digital health siyo tu kuwa na computer au kutumia smartphone kazini.

WHO inaeleza digital health kwa mtazamo mpana zaidi—technology inapaswa kusaidia health systems kutoa huduma bora, zinazofikika na zenye usawa.

Kwa hiyo healthcare professional mwenye digital skills siyo lazima awe programmer.

Anahitaji kuelewa technology inavyotumika ndani ya healthcare na namna ya kuitumia kwa usahihi.

Kwa nini digital skills ni muhimu kwa healthcare professionals?

Healthcare professionals wanaanza kukutana na technology katika sehemu nyingi zaidi za kazi zao.

Unaweza kuwa unatumia electronic records.

Unaweza kushiriki kwenye telehealth.

Unaweza kutumia digital tools kwa patient education.

Unaweza kufanya kazi na healthcare data.

Au unaweza kuwa sehemu ya project inayohusisha implementation ya digital health system.

Research ya hivi karibuni inaonyesha kwamba digital competence inatofautiana sana miongoni mwa healthcare professionals, na kwamba training, organisational support na leadership vinaweza kuhusika katika maendeleo ya competence hiyo. Utafiti wa 2026 uliohusisha healthcare professionals kutoka nchi na maeneo 19 ulitambua makundi tofauti ya digital competence, kuanzia beginners hadi “pioneers.”

Kwa hiyo siyo kwamba kila healthcare professional anatakiwa kujua kila digital tool.

Lakini kujua kiwango chako na kujua skills gani unahitaji kuongeza ni muhimu.

Skills 7 za Digital Health ambazo healthcare professionals wanapaswa kuanza kujifunza

1. Digital Health Literacy

Hii ndiyo foundation.

Digital health literacy ni zaidi ya kujua kutumia computer.

Ni uwezo wa kuelewa, kutumia na kutathmini information na technologies zinazohusiana na healthcare.

Kwa mfano:

Unaweza kupata health information online.

Je, unaweza kutambua kama source ni credible?

Unaweza kutumia digital system.

Je, unaelewa namna information inavyoingizwa na kutumika?

Unaweza kutumia digital tool.

Je, unaelewa limitations zake?

Hii ni muhimu sana kwa healthcare kwa sababu information isiyo sahihi inaweza kuathiri decision-making na patient care.

Na hii si theoretical issue kwa Tanzania.

Utafiti uliofanywa kwa primary-care workers Tanzania, ukiwahusisha nurses, clinical officers na community health workers, ulionyesha tofauti katika namna digital health literacy inavyoeleweka na kutumika. Utafiti huo pia ulihusisha digital health literacy na data quality, continuity of care na patient communication.

Kwa hiyo digital health literacy ni skill ambayo healthcare professional wa Tanzania anaweza kuhitaji sasa, not someday.

2. Data na Health Information Management

Healthcare ina data nyingi.

Patient records.

Laboratory results.

Appointments.

Treatment information.

Health statistics.

Research data.

Na data hiyo inahitaji kushughulikiwa kwa usahihi.

Healthcare professional anapaswa angalau kuelewa basics za:

  • Data collection

  • Data quality

  • Data interpretation

  • Health information systems

  • Data privacy

  • Basic data reporting

Huhitaji kuwa data scientist.

Lakini ukiweza kuelewa data inayotumika katika healthcare, unakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kufanya decisions na kushirikiana na teams zinazofanya kazi na health information systems.

3. Telehealth na Virtual Care

Telehealth imebadilisha namna baadhi ya healthcare services zinavyoweza kufikishwa kwa patients.

Lakini kuna misconception moja:

Telehealth siyo tu kufanya consultation kupitia video call.

Healthcare professional anayefanya kazi katika virtual environment anahitaji kuelewa communication, technology, patient safety, documentation na professional responsibilities.

A 2026 scoping review ya telehealth education na competencies ilionyesha umuhimu wa kuandaa healthcare professionals kwa virtual care na kuendeleza competencies zinazohitajika katika mazingira hayo.

Kwa hiyo kama una interest kwenye telehealth, usijifunze kutumia Zoom pekee.

Jifunze Ni jinsi gani healthcare inafanya kazi katika virtual environment.

Na bila shaka, mara zote zingatia professional licensing, scope of practice, privacy na regulations zinazotumika katika jurisdiction husika.

4. Health Information Systems

Healthcare organizations zinatumia systems kuhifadhi na kusimamia information.

Hapa unaweza kukutana na:

Electronic Health Records (EHRs)

Hospital Information Systems

Laboratory Information Systems

Pharmacy systems

Appointment systems

Na systems nyingine za health information.

Healthcare professional anayeelewa workflow ya clinical environment ana advantage anapofanya kazi na systems hizi.

Kwa nini?

Kwa sababu technology inapaswa ku-support healthcare workflow—not kufanya workflow iwe ngumu zaidi.

Hapo ndipo healthcare knowledge yako inakuwa valuable kwa digital health teams.

5. AI Literacy

Hii ni moja ya skills ambazo healthcare professionals hawawezi kupuuza.

Lakini AI literacy siyo kujua kuandika prompts za ChatGPT tu.

Healthcare professional anahitaji kuelewa:

  • AI inaweza kufanya nini

  • AI haiwezi kufanya nini

  • AI inaweza kufanya errors gani

  • Jinsi ya ku-verify AI-generated information

  • Privacy na confidentiality

  • Human oversight

  • Ethical use of AI

Pia soma:

WHO imeendelea kusisitiza umuhimu wa responsible use of AI katika health, ikiwa ni pamoja na usalama, privacy, transparency, accountability na human oversight.

Kwa hiyo unaweza kutumia AI kukusaidia kwenye research, writing, summarisation au workflow.

Lakini kwenye healthcare:

AI output siyo automatically medical truth.

Verification bado ni muhimu.

6. Digital Communication

Hii mara nyingi watu wanaipuuzia.

Lakini healthcare communication inabadilika.

Unaweza kuwasiliana na patient kupitia:

  • Patient portals

  • SMS

  • Email

  • Telehealth platforms

  • Social media

  • Websites

  • Digital education materials

Kujua medical information pekee hakutoshi.

Unahitaji kujua jinsi ya kuwasilisha information hiyo kwenye digital environment.

Hii ndiyo sehemu ambayo healthcare professionals wanaweza kuchanganya medical knowledge na skills kama:

Medical writing + SEO + content marketing + patient education.

Na hapo ndipo career paths mpya zinaweza kuanza.

7. Digital Professionalism

Kuwa online kama healthcare professional kunahitaji responsibility.

Unapaswa kufikiria kuhusu:

  • Patient confidentiality

  • Professional boundaries

  • Privacy

  • Medical misinformation

  • Ethical content

  • Digital footprint

Kwa mfano, kama unaandika health content online, siyo kila claim inayopata engagement ndiyo claim unapaswa kutumia.

Healthcare content inahitaji accuracy kabla ya virality.

Hii ni tofauti kubwa kati ya content marketing ya kawaida na healthcare content marketing.

Je, unahitaji kujifunza skills zote hizi?

Hapana.

Na hapa ndipo watu wengi wanapokosea.

Unaweza kuona list hii na kusema:

“Sasa mimi nitajifunza AI, data, telehealth, SEO, EHR, programming… yote kwa pamoja?”

No.

Anza na skill combination inayolingana na career direction yako.

Kama unapenda Medical Content:

Healthcare + Medical Writing + SEO + Research + AI

Kama unapenda Digital Health:

Healthcare + Health Information Systems + Data + Digital Health

Kama unapenda Telehealth:

Healthcare + Telehealth + Digital Communication + Patient Safety

Kama unapenda Healthcare Marketing:

Healthcare + Content Marketing + SEO + Analytics + Patient Education

Kama unapenda Healthcare Data:

Healthcare + Data Literacy + Health Information Systems + Analytics

Hii ndiyo concept muhimu:

Usijenge digital skills bila direction.

Jenga skills zinazoongeza value kwenye knowledge ambayo tayari unayo.

Na hii ina maana gani kwa healthcare professionals Tanzania na Kenya?

Hapa ndipo conversation inakuwa interesting.

Mara nyingi tunapozungumzia remote work, tunafikiria software developers, graphic designers, virtual assistants au digital marketers.

Lakini healthcare professionals’ pia wana knowledge ambayo inaweza kutumika katika digital economy.

Mfano:

Clinical Officer anaweza kuongeza medical writing na digital health skills.

Nurse anaweza kuongeza telehealth, patient education au health information skills.

Pharmacist anaweza kuingia kwenye medical content, health-tech support au medication information projects.

Public health professional anaweza kuongeza data, research na digital communication skills.

Healthcare professional mwenye interest kwenye marketing anaweza kujifunza healthcare content marketing na SEO.

Hii haimaanishi kwamba kila mmoja atapata remote job automatically.

Digital skills si shortcut ya kupata kazi.

Lakini zinakupa uwezo wa kuchanganya healthcare expertise yako na mahitaji mapya ya digital healthcare.

Uanze wapi kama huna digital skills nyingi?

Usianze kwa kununua courses 10.

Anza na basics.

Month 1: Digital foundation

Jifunze:

  • Digital health basics

  • Data privacy basics

  • Digital communication

  • Basic health information systems

Month 2: Chagua specialization

Chagua moja:

Medical Content au Digital Health au Telehealth au Healthcare Data au Healthcare Marketing

Month 3: Build something

Hii ndiyo step ambayo watu wengi wanaruka.

Usikusanye certificates tu.

Tengeneza kitu.

  • Write an evidence-based healthcare article.

  • Build a small healthcare content calendar.

  • Analyze healthcare website data.

  • Create a patient education resource.

  • Research a digital health topic.

  • Build a small portfolio.

Show what you can do.

Future ya healthcare professional siyo tu clinical

Healthcare bado inahitaji strong clinical professionals.

Lakini healthcare systems nazo zinabadilika.

Technology inabadilika.

Patient expectations zinabadilika.

Na skills zinazohitajika nazo zinabadilika.

Kwa hiyo usifikirie:

“Digital skills ni za watu wa IT tu.”

Fikiria:

“Ninawezaje kutumia digital skills kuongeza value ya healthcare knowledge yangu?”

Hilo ndilo swali bora zaidi.

Kwa sababu huenda future yako isiwe kuchagua kati ya healthcare au technology.

Huenda ikawa:

Healthcare + Technology.

Na hapo ndipo opportunities mpya zinaanza.

What digital health skill are you learning?

Kama wewe ni healthcare professional, tuambie kwenye comments:

Ni skill gani ungependa kuongeza—AI, Telehealth, Healthcare Data, Medical Writing, SEO au Digital Health?

Na kama tayari umeanza kujifunza moja, niambie umeanza na ipi na kwa nini.

Huenda comment yako ikawa topic ya article yetu inayofuata.

About the Author

Fatuma Ramadhani is a healthcare professional and content marketing specialist with an interest in the intersection of healthcare, digital health, medical content, and remote work.

She combines healthcare knowledge with skills in content strategy, SEO, analytics, and digital communication to create healthcare content that is clear, evidence-based, and useful to everyday readers.

Through her work in healthcare and digital content, she explores how healthcare professionals can build relevant digital skills and adapt to the changing world of work.

Connect with Fatuma Ramadhani: https://www.linkedin.com/in/fatuma-ramadhani